Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558304

Habari za michezo of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Balozi Bana: Yanga Pindueni meza mara tano

Balozi Bana: Yanga Pindueni meza mara tano Balozi Bana: Yanga Pindueni meza mara tano

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk Benson Bana ametua katika hoteli ya Yanga kisha akawaachia ujumbe mzito wachezaji.

Yanga iko nchini Nigeria jijini Port Harcourt ambapo kesho watashuka Uwanja wa Adokie Amiesimaka katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao Rivers United.

Akizungumza na wachezaji muda mchache uliopita Balozi Bana amesema amefurahishwa na kauli mbiu ya Yanga kuelekea mchezo huo ya kupindua meza akisema anataka kuona meza hiyo inapinduliwa mara tano.

Balozi Bana amesema amesema amekuwa akipokea simu nyingi za viongozi mbalimbali wa nchini Tanzania wakitaka kujua maendeleo ya Yanga na kwamba matokeo mazuri yatawafurahisha Watanzania wote.

"Karibuni sana hapa Nigeria mjisikie mko huru mcheze kwa nguvu kuipigania Tanzania,nimefurahishwa na msemo wenu mkisema mmekuja kupindua meza sasa mimi nawataka mkapindue meza mara tano," amesema Balozi Bana.

"Nendeni kesho mkijua kwamba sisi Watanzania tuliopo hapa na wale tuliowaacha nyumbani wanataka ushindi sina wasiwasi na uwezo wenu.

Aidha Balozi Bana ameongeza kwamba kutokana na umbali wa makazi yake ya ubalozi na mji ambao kikosi umefikia ameamua kuweka kambi Portharcourt ili aweze kushuhudia mchezo huo.

"Mimi ni Yanga damu nilikuwa na kikao na mabalozi wenzangu kwa njia ya mtandao nikawaambia nitakuwa natoka kila wakati nina ugeni wa timu yangu ya Yanga na kila wakati nataka kujua wanaendeleaje.

"Sitaweza kurudi kule kwangu na nitabaki hapa mpaka mtakapocheza tuwashangilie na serikali inataka kuona mnashinda sasa kafanyeni kweli,"