Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 10Article 541981

Habari za michezo of Thursday, 10 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Banda: Mfumo wa Gomes Utanibeba Simba

Banda: Mfumo wa Gomes Utanibeba Simba Banda: Mfumo wa Gomes Utanibeba Simba

KUFUATIA kukiri kuwa Uongozi wa Simba tayari umefanya mazungumzo na uongozi wake, beki wa Klabu ya Simba, Abdi Banda amefunguka kuwa kama dili hilo litakamilika anaamini mfumo wa Kocha wa Simba, Didier Gomes utamsaidia kupata nafasi licha ya changamoto kubwa ya ushindani wa namba kwenye kikosi hiyo.

Banda mwenye umri wa miaka 26, alikipiga ndani ya Klabu ya Simba kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 na kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Klabu ya Highlands ya nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Championi Jumatano, Banda alisema: “Najua ndani ya kikosi cha Simba kwa sasa kumekuwa na ushindani mkubwa wa namba hasa katika nafasi ya ulinzi, lakini kama mchezaji lazima ujiandae kwa changamoto yoyote.

“Hivyo, kama itatokea nikasajiliwa nao naamini ninaweza kupata nafasi ya kucheza kutokana na juhudi zangu binafsi kama mchezaji kulishawishi benchi la ufundi na kwa mfumo wa kocha Gomes wakuanza na walinzi wanne.”

Join our Newsletter