Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 13Article 551302

Habari za michezo of Friday, 13 August 2021

Chanzo: ippmedia.com

Banda akabidhiwa mikoba Simba SC, ratiba CAF ikitoka

Banda akabidhiwa mikoba Simba SC, ratiba CAF ikitoka Banda akabidhiwa mikoba Simba SC, ratiba CAF ikitoka

Banda ambaye amejiunga na Simba wiki iliyopita amemaliza tetesi za hatima ya Miquissone ambaye dili lake la Al Ahly lilikuwa halijawekwa hadharani na klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Nyota huyo jana alionekana akiwa amevaa jezi hiyo wakati wakielekea kwenye mazoezi ya timu yao iliyoweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika yatakayoanza mapema mwezi ujao.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema anashangaa kuona baadhi ya waandishi na wachambuzi wa habari wanaulizia dili la Miquissone limefikia hatua zipi, wakati klabu hiyo haijawahi kutamka popote pale kuwa imepata ofa ya kumuuza mchezaji huyo.

"Usajili unamalizika terehe 15, kwa hiyo nawasihi wanachama na mashabiki wa Simba kuwa watulivu, kama kuna lolote lile tutawaambia, lakini kwa sasa hakuna kitu kama hicho," alisema Kamwaga.

Kamwaga pia amewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kujiandaa na tamasha la Wiki ya Simba, maarufu kama Simba Day ambalo litafanyika Agosti 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini.

Wakati huo huo wapinzani wa Simba na Yanga katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wanatarajiwa kujulikana katika ratiba ya michuano hiyo inayosimamiwa na kuandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), itakayotolewa leo jijini Cairo.

Pia Azam FC na Biashara United ya Mara zitawafahamu wapinzani wao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika inayotarajiwa kushirikisha timu 51 itakapowekwa hadharani leo jijini humo.