Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559939

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Bao la Mayele Sh400 Milioni

Fiston Mayele Fiston Mayele

BAO lililofungwa na Fiston Mayele dakika ya 12 ya mchezo wa Ngao ya Jamii, juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, limewahakikisha mastaa wa Yanga kuvuna Sh 400 milioni kama bonasi toka kwa matajiri wao, straika huyo Mkongoman akiwa na uhakika wa kupata Sh20 Milioni.

Alhamisi baada ya mazoezi bosi wa timu hiyo, Ghalib Said alitoa ahadi ya kuwapa mastaa hao, Sh 400 Milioni kama wataifunga Simba na kwamba mfungaji wa bao angelamba peke yake Sh 20 milioni ikiwa na maana Mayele tayari ana uhakika wa kuibeba fedha hiyo.

Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mbatha aliliambia Mwanaspoti motisha kwa wachezaji imetumika ikiwa ni sehemu ya kuchagiza ushindi wa mchezo huo na kwamba kwa sasa wanaelekeza nguvu kwenye mechi za Ligi Kuu Bara inayoanza leo na Yanga ikianzia Bukoba kucheza na Kagera Sugar.

Senzo alisema msimu wana kikosi kizuri chenye ushindani wa wao kwa wao na anaamini watakuwa na msimu mzuri kuliko yote.