Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 13Article 557143

Habari za michezo of Monday, 13 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Barakoa zatolewa bure Karimjee wakimuaga Hans Poppe

Barakoa zatolewa bure Karimjee wakimuaga Hans Poppe Barakoa zatolewa bure Karimjee wakimuaga Hans Poppe

KUTOKANA na janga la virusi vya corona uongozi wa Simba umetoa barakoa bure kwa ajili ya waombolezaji wanaokuja kushiriki ibada ya msiba wa aliyekuwa Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba Zacharia Hans Poppe.

Hans Poppe alikutwa na umauti Septemba 10 wakati akitibiwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa zaidi ya wiki moja.

Martine maarufu Simba Boy ambaye alikuwa sehemu ya watoa barakoa amesema wameelekezwa kuzitoa bure kwa waombolezaji.

Mbali na Barakoa kutolewa bure katika geti la kuingilia lakini bado wajasiliamali wa biashara hiyo walikuwepo kwa ajili ya kuuza.

MWILI UMEWASILI Mwili wa Poppe umewasilia viwanja vya Karimjee majira ya saa 10:46 asubuhi na kupokelewa na viongozi wa Simba wakiongozwa na Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez.

Baada ya kuwasili bodi nzima wa wakurugenzi ya Klabu hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wao Salim Abdallah 'Try Again' waliongoza zoezi la kuutoa mwili kwenye gari lililoleta mwili.

Mjumbe wa Bodi Cresentius Magoli ndiye mshereheshaji katika ibada hii muhimu kwa mpendwa wao anayetarajiwa kupumzishwa katika nyumba yake ya milele Jumatano Mkoani Iringa.

NYONGEZA NA LEONARD MUSIKULA