Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 08Article 584338

Soccer News of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Barca bado yajikongoja La Liga

Barca yalazimishwa sare Barca yalazimishwa sare

Barcelona imelazimishwa sare ya goli 1-1 na Granada katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga huku beki wa kulia Dani Alves akirejea na kutoa asisti kwenye mechi yake ya kwanza La Liga.

Kukosa ushindi kuinaifanya Barcelona kupoteza nafasi ya kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo.

Alves alitoa msaada wa goli baada ya kupiga krosi kwa Luuk de jong wakati bao la kusawazisha lilitokea kunako dakika ya 89 likifungwa na Antonio Puertas.

Kwenye mechi hiyo pia imeshuhudiwa mchezaji mmoja wa Barcelona Gavi akionyeshwa kadi nyekundu hivyo kulazimika kumaliza pungufu.

Barcelona watacheza mechi ijayo dhidi ya Real Madrid katika nusu fainali ya Super Cup.