Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 30Article 560458

Soccer News of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Barca yachapwa 3 UEFA, Kocha atajwa

Mechi baina ya Benfica dhidi ya Barcelona Mechi baina ya Benfica dhidi ya Barcelona

Jinamizi la matokeo mabaya bado linaendela kukikumba kikosi cha Barcelona baada ya usiku wa jana kupoteza ugenini dhidi ya Benfica.

Katika mchezo huo wa kundi E, Barcelona walishuhudia wakipoteza kwa magoli 3-0 kutoka kwa Benfica na kuwafanya kupoteza mchezo wa pili mfululizo katika Kundi lao.

Barcelona walijikuta wakimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki wake Eric Garcia kuonyeshwa kadi nykundu dakika za mwishoni mwa mchezo huo.

Magoli ya benfica yamefungwa na D. Nunez 3',R. Silva 69 kisha D. Nunez akarudi tena kwa mkwaju wa Penati 79'.

Kipigo hicho kinazidi kusafisha njia kwa Mwalimu Ronald Koeman kuelekea kutimuliwa kwani tayari kuna tetesi znazoeleza mabosi wa Klabu hiyo na hasa Rais Laporta hawaridhishwi na mbinu zake.

Katika mechi nyingine ya kundi hiloBayern Munich walishinda magoli 5-0 dhidi ya Dynamo Kyiv.