Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 22Article 558919

Soccer News of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Beki Simba aahidi makubwa

Beki wa Simba, Henock Inonga Baka Beki wa Simba, Henock Inonga Baka

Beki mpya wa wekundu wa msimbazi, Mkongomani, Henock Inonga Baka, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kumuamini kwa kipindi ambacho atakuwepo hapo, huku akiahidi kutimiza malengo ya timu hiyo ambayo ni kubeba makombe.

Inonga amejiunga na Simba msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea DC Motema Pembe ya DR Congo.

Katika moja ya majiano yake, Baka amesema ana mengi ya kuwafanyia Simba, lakini kikubwa anaomba sapoti ya mashabiki huku akifahamu kwamba ni ngumu mchezaji mgeni kuaminika moja kwa moja.

“Nimejiunga na moja ya timu kubwa Afrika ambayo ina wachezaji wengi wakubwa wenye uwezo wa kimataifa.

“Ili mchezaji ufanye vizuri, lazima kwanza uaminike kwa mashabiki, hivyo niwaombe waniamini ili niifanyie makubwa timu yangu mpya ya Simba.

“Nafahamu ushindani uliopo katika timu, hivyo nitahakikisha ninapambana ili kufanikisha malengo ya timu kubeba makombe katika kuelekea msimu ujao,” amesema Baka.

Inonga anatarajiwa kukutana na ushindani mkubwa wa namba kutoka kwa Wawa na Mkenya Joash Onyango ambao msimu uliopita kombinesheni yao imeonekana kuzaa matunda.