Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 18Article 552103

Soccer News of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Beki Yanga arejea kupamabia namba

Beki wa Yanga, Yassin Mustapha Beki wa Yanga, Yassin Mustapha

Beki wa Yanga, Yassin Mustapha amesema kitendo cha kuanza kufanya mazoezi ni jambo zuri kwake kwani anaamini anarudi kwenda kutetea namba yake katika kikosi cha kwanza.

Yassin alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuwa majeruhi na nafasi yake ilichukuliwa na Adeyum Saleh ambaye alionyesha kiwango kizuri msimu uliopita na pia Yanga tayari imemsajili David Bryson kutoka KMC kuja kucheza nafasi hiyo.

Akizungumza na mmoja wa Waandishi wa habari, Yassin amesema tayari ameshaanza mazoezi madogo madogo na hana maumivu yoyote yale na anasubiri programu za mwalimu na kuzitekeleza.

“Si unaona nasafiri na wenzangu hapa kwenda kujianda na msimu mpya, acha nikapambane maana nimekaa nje kwa muda kidogo kwahiyo kuna kazi ya kufanya kurejea katika hali yangu,”

“Majeraha niliyoyapata yamenirejesha nyuma kidogo ila kikubwa nimeanza kupona na nilishaanza mazoezi binafsi basi tuombe Mungu atajaalia, “ amesema Yassin.

Beki huyo alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Polisi Tanzania na moja kwa moja aliingia katika kikosi cha kwanza na kufanya aitwe katika timu ya Taifa Tanzania.

Baada ya kucheza nusu msimu mshambuliaji huyo alipata majeraha ya mguu na kufanya akose nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha Stars kilichocheza mechi ya Kirafiki na Malawi.