Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585910

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Benitez: Lucas Digne ilikuwa ni Biashara nzuri

Lucas Digne na Benitez Lucas Digne na Benitez

Kocha wa timu ya Everton Rafael Benitez amesisitiza kwamba kuondoka kwa Lucas Digne ni biashara mzuri kwa klabu yake ya Everton.

Mlinzi huyo wakushoto kutokea taifa la Ufaransa amejiunga na klabu ya Aston Villa kwa uhamsho uliogharimu kiasi cha Pauni milioni 25 baada ya kupoteza matumaini akiwa chini ya Benitez kwenye viunga vya Goodison Park.

Benitez alinukuliwa akisema, “ni jambo zuri, kumbadilisha mchezaji ambaye alikuwa anafikisha miaka 29 na wachezaji vijana, mimi ni kocha na nawajibuika na maamuzi yangu, ni muda wakuifikilia timu na mipango ya baadae, inabidi tusonge mbele.”

Digne ambaye amesaini mkataba wamiaka minne na nusu na klabu ya Aston Villa alisema kuwa hakutarajia kuondoka kama alivyoondoka kwenye viunga vya Goodison Park huku akimtuhumu kocha wake.

“Ni mtu mmoja wa kutoka nnje ambaye ataharibu mapenzi yako” alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.