Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 586126

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Benzema : Sipendi Soka la aina hii

Mshambuliaji wa Madrid Karim Benzema Mshambuliaji wa Madrid Karim Benzema

Kwa mujibu wa Marca, Karim Benzema amechaguliwa kama mchezaji bora wa mwaka 2021 Ufaransa.

Nyota huyu anaamini kuwa kumekuwa na kasoro katika namna ya kutazama nani ni mchezaji bora.

Yeye anadhani kuna haja ya kutazama zaidi mchango wa mchezaji na kile anachofanya uwanjani zaidi ya kutazama magoli pekee.

Akihzungumza katika mahojiano na chanzo kimoja cha habari cha Ufaransa, amenukuliwa akisema;

“Ukiachana na takwimu za kufunga magoli mengi, sijaona kingine kilichobadilika kwenye soka langu. Mimi mi mchezaji yule yule, hatuhangaiki kuangalia tena nini mchezaji anafanya uwanjani, ni yule aliyefunga tu. Na kifuatacho huyo anakuwa mchezaji bora” – Benzema

“Imenitokea mimi. Sichezi mpira mzuri sana lakini ninafunga na wananiona mimi kama bora. Sipendi sana aina hii ya soka, lakini itaendelea kuwa hivi zaidi na zaidi. Imekuwa ni mchezo wa kuangalia takwimu tu” – Benzema

Benzema mekuwa na mchango mkubwa sana kwa Real Madrid kufanya vyema kwa sasa, wakiwa na pointi tano zaidi kileleni.