Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 09Article 584455

Soccer News of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Benzema afukuzia rekodi ya Ronaldo Madrid

Mshambuliaji wa Madrid Karim Benzema Mshambuliaji wa Madrid Karim Benzema

Kwenye ushindi wa goli 4-1 ambao Real Madrid wameupata dhidi ya Valencia huku mshambuliaji wa kati wa timu hiyo akifunga bao mbili na kuisaidia timu hiyo kushinda yanamfanya kufikisha goli 301 katika mechi 584.

Benzema alifunga goli mbili kwa njia ya penati la kwanza ni pale ambapo kiungo mkabaji wa Brazil Casemiro alifanyiwa madhambi kwenye eneo hatari kabla ya bao la pili.

Baada ya kufunga goli hizo, sasa Benzema anakuwa amepitwa na wachezaji watatu ambao wanabao nyingi Real Madrid Cristiano Ronaldo(450), Raul (323) na Alfredo Di Stéfano(308).

“Ni furaha kubwa kwangu”, alisema Benzema. “Kufunga idadi ya goli hizo katika timu hii najiona mwenye furaha, hii ni klabu kubwa nilikuwa natakiwa kufanya makubwa”.

Magoli mengine kwenye mechi hiyo yamefungwa na winga Vinicius Junior ambapo sasa wanaenda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga kwa tofauti ya alama nane na timu iliyonafasi ya pili Sevilla.