Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 20Article 558532

Soccer News of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Biashara United kuhamishia ubora Ligi kuu

Kikosi cha Biashara United Kikosi cha Biashara United

Wanajeshi wa Mpakani, Biashara United kwa sasa wanatamba baada ya kumaliza kazi ya dakika 180 kwenye mechi ya awali.

Biashara United iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ilipokuwa ugenini dhidi ya DIKHIL na ule wa pili uliochezwa Uwanja wa Azam FC ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Ramadhan Chombo wengi wanapenda kumuita Redondo.

Kocha wa Biashara United Patrick Odhiambo amesema kuwa vijana wake wanastahili pongezi kwa kuwa walipambana bila kukata tamaa mwanzo mwisho.

"Wachezaji walikuwa katika hali nzuri na wamepambana kwa ajili ya kupata matokeo chanya na mwisho wa siku wamefanikiwa kupata kile ambacho wanakihitaji.

"Bado kuna kazi kubwa na tunahitaji kupata matokeo hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kila kitu kitakuwa sawa," amesema

Kwa sasa Biashara inajiandaa vyema na Mechi ya Ligi kuu dhidi ya Simba, ambapo ligi hiyo inatarajiwa kuanza Septemba 27.