Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 07Article 555892

Soccer News of Tuesday, 7 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Biashara United safarini kuwafuata FC Dikhil

Kikosi cha Biashara United Kikosi cha Biashara United

Kikosi cha Biashara United ‘Wanajeshi wa Mpakani’ kinatarajia kuondoka alfajiri ya kesho kuelekea nchini Djibouti kwa ajili ya mchezo wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya FC DIKHIL.

Timu ya Biashara inakwenda kucheza mchezo wa awali wa kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika, mchezo ambao utachezwa Septemba 10 majira ya saa 9:00 Alasiri.

Katibu wa Biashara United Frank Wabare amesema, msafara utakuwa na jumla ya watu 30, ambapo wachezaji 20 pamoja na viongozi 10.

Biashara United leo imefanya mazoezi asubuhi kwenye uwanja wa Uhuru, Dar ikiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya safari.

Mechi hiyo itapigwa katika Uwanja wa Stade du Ville na haijawekwa wazi kama mashabiki wataruhusiwa kutokana na Changamoto za Corona ama la.

Tanzania itawakilishwa na timu nne (4) zinazokwenda kushiriki mashindano ya kimataifa, Simba na Yanga watashiriki Klabu bingwa Afrika huku Biashara na Azam FC watashiriki Kombe la Shirikisho.