Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 17Article 558004

Soccer News of Friday, 17 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Biashara kukipiga Chamazi bila Mashabiki

Kikosi cha Biashara United kikiendelea kujifua Kikosi cha Biashara United kikiendelea kujifua

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limekataa maombi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuruhusu Mashabiki kwenye mechi kati ya Biashara United na FC Dikhil ya Djibouti.

Mechi hiyo ya marudiano ya Kombe la Shirikisho la CAF itachezwa Jumamosi, Septemba 18 mwaka huu saa 1 kamili jioni Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

CAF imesisitiza kuwa mechi zake zote zitachezwa bila Mashabiki kama ilivyoainishwa katika mwongozo wake na ule wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusu ugonjwa wa Covid-19.

Sehemu ya taarifa ya TFF