Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584803

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Bila Aubameyang, Gabon yaanza vyema AFCON

Wachezaji wa Gabon wakishangilia golidhidi ya Comoro Wachezaji wa Gabon wakishangilia golidhidi ya Comoro

Aaron Boupendza alijaza pengo la Pierre-Emerick Aubameyang ambaye ana virusi vya corona na kuipa Gabon ushindi wa 1-0 dhidi ya wageni wa Kombe la Mataifa ya Afrika Comoro hapo jana mjini Yaounde.

Taifa hilo la visiwa vya bahari ya Hindi ni moja ya timu mbili zinazoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza pamoja na Gambia. Gabon wanashiriki kwa mara ya nane.

Walifuzu mara mbili katika hatua ya nane za mwisho, katika mwaka wa 1996 na 2012.

Ushindi wa Gabon una maana vijana hao wa kocha Patrice Neveu wana pointi tatu sawa na Morocco, ambao waliwafunga Ghana bao moja kwa sifuri mapema jana katika mechi nyingine ya Kundi C. Katika Kundi B, Guinea iliifunga Malawi moja bila kupitia bao la dakika ya 35 lake Issiaga Sylla katika mji wa magharibi wa Bafoussam na kukamata nafasi ya kwanza pamoja na Senegal.

Senegal walipata ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Zimbabwe katika mechi ya kwanza jana kupitia bao la penalti iliyopigwa na Sadio Mane kunako dakika ya 97.