Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 30Article 540628

Habari za michezo ya

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Bilionea GSM aimwagia sifa Azam

Bilionea GSM aimwagia sifa Azam Bilionea GSM aimwagia sifa Azam

Bosi wa kampuni ya GSM inayoidhamini Yanga, Ghalib Said Mohamed amepongeza mkataba wa udhamini wa haki za matangazo ya Ligi Kuu baina ya Kampuni ya Azam Media Limited na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliosainiwa Jumanne iliyopita jijini Dar es Salaam wenye thamani ya Sh 225.6 bilioni.

Mkataba huo wa miaka 10 utaanza katika msimu ujao wa Ligi mara baada ya huu wa sasa wenye thamani ya Sh 23 bilioni kwa miaka mitano kumalizika mwishoni mwa msimu unaoendelea.

Bosi huyo wa GSM amesema kuwa mkataba huo utatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya mchezo wa soka na pia kuongeza ajira nchini.

Binafsi nichukue fursa hii kuwapongeza kwa dhati ya moyo wangu wangu Azam Media Limited. wamekuza thamani ya Ligi yetu, wamevitendea haki vilabu kwenye mapato, wamewatendea haki Watanzania kuonyesha karibu 99% ya mechi zote za Ligi Kuu.

Hii inatoa fursa kwa vijana wetu wa Kitanzania kuonyesha vipaji vyao ndani ya mipaka ya nchi na hata nje.

Aidha ni wajibu wetu kama Watanzania kuwaunga mkono na kuwapongeza Azam Media Limited," aliandika Gharib.

Join our Newsletter