Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 03Article 540796

xxxxxxxxxxx of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Bocco, Manula waiamsha Azam

Dube amesaini mkataba miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin `Popat` alisema hawafikirii kumuuza Dube na hata mchezaji yoyote yule ambaye yuko katika mipango ya kocha wao, George Lwandamina.

Popat alisema hatuwezi kurudia makosa ya nyuma ambayo walimuuza Kipre Tcheche ila hali hawakupata mbadala wake na kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea ikiwamo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kimataifa.

“Kwa msimu huu hatuuzi mchezaji labda msimu ujao, maana tukirudi nyuma tunakumbuka jinsi tulivyoyumba kipindi tulichomuuza Kipre bila ya kuwa na mbadala wake na kushindwa kufanya vizuri, sasa hatutakuwa litokee kwa Dube,”.

“Tuna jicho moja halafu hilo hilo tulitoe, hatutakubali kwa sababu sasa mipango yetu ni kujenga timu imara kwa ajili ya kuimarisha kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao,” alisema Popat.

Aliongeza wataendelea kufuata mapendekezo ya Lwandamina kwa kuhakikisha wanawabakisha wachezaji wanaokaribia kumaliza mikataba yao ili wasije kuondoka kama ilivyotokea kwa John Boccn, Aishi Manula na Erasto Nyoni ambao sasa wanang'ara katika kikosi cha Simba.

Join our Newsletter