Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585823

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Bocco: Tulieni, bado mawili

Nahodha John Bocco Nahodha John Bocco

Nahodha wa Simba, John Bocco amesema wamefungua mwaka vizuri kwa kutwaa taji la Mapinduzi wanatarajia kutetea mawili yaliyobaki.

Simba wametwaa taji hilo baada ya kumfunga Azam FC bao 1-0 iliwa ni fainali yao ya tatu kukutana na wao kuibuka na ubingwa baada ya kushindwa mara mbili.

Bocco anasema baada ya kushindwa kuwafunga ndani ya misimu miwili waliyokutana fainali walikuwa na mbinu nyingine kuhakikisha wanatwaa taji.

“Haikuwa rahisi lakini ubora na uzoefu umetubeba na kufanikisha hili tunaangalia mipango mingine ya mataji yaliyobaki kwa kuhakikisha tunayatetea,” anasema.

“Azam FC walicheza vizuri lakini hawakuwa bora kama tulivyokuwa bora kitu kilichosaidia sisi kupata matokeo ambayo yametupa taji la nne,” anasema na kuongeza kuwa;

“Habari za taji sasa tumelisahau tunaangalia namna ya kutetea taji la ligi kuu ambalo tumelitwaa mara nne mfululizo na tunaimani tunaweza kutokana na matarajio na morali kwa wachezaji,” anasema.