Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 26Article 559720

Soccer News of Sunday, 26 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Bocco awapongeza Yanga

Washindi ngao ya Jamii 2021/2022 Washindi ngao ya Jamii 2021/2022

Nahodha wa Simba John Bocco 'Adebayo' licha ya timu yake kufungwa amewapongeza wapinzani wao kwa mchezo mzuri walioucheza.

Simba alikuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa ngao ya Hisani uliopigwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambao Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Fiston Mayele.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Bocco amewapongeza Yanga kwa namna ambavyo walikuwa na mchezo mzuri hasa kipindi cha pili na kufanikiwa kulitwaa taji hilo ambao wao walikuwa wakilitetea.

"Namshukuru sana Mungu kwa kumaliza mchezo salama, na pia nawapongeza wapinzani wetu kwa mchezo mzuri na kutumia vyema nafasi walizozipata kushinda mchezo huo,"amesema.

Aidha Bocco amesema hata wao walitamani kupata matokeo katika mchezo huo lakini bahati haikuwa upande wao hivyo hawana budi kukubali matokeo kwa kuwa ilikuwa ni lazima mshindi apatikane.

Bocco amesema sasa kwa sasa wanageukia ligi pamoja na michuano ya Ligi ya Mabingwa huku akiwataka wanasimba kukaa mkao wa kula kuelekea michezo ijayo kwa kuwa ngao ya hisani imepita.