Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 12Article 557017

Soccer News of Sunday, 12 September 2021

Chanzo: salehejembe.blogspot.com

Bodi ya Ligi yafafanua kuhusu Mpango wa V.A.R Ligi kuu 2021/2022

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo play videoAfisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo

Ikiwa tayari ratiba ya Ligi Kuu Bara ipo wazi na inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 27.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) imeweka wazi kwamba kwa sasa haina mpango wa kuleta V.A.R na badala yake itawekeza kuwawezesha waamuzi kuwa na mawasiliano zaidi ili kuweza kupunguza changamoto za waamuzi wanaposimamia sheria 17 zinazoongoza mchezo wa Soka.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo wakati akifanya mahojiano na moja ya vyombo vya habari hapa nchini.