Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 20Article 547771

Habari za michezo of Tuesday, 20 July 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Bodi ya Ligi yafunguka ishu ya Mwenyekiti Simba kutovaa medali

Bodi ya Ligi yafunguka ishu ya Mwenyekiti Simba kutovaa medali Bodi ya Ligi yafunguka ishu ya Mwenyekiti Simba kutovaa medali

GUMZO lililopo hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii ni kutoitwa na kuvalishwa medali ya ubingwa kwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Murtaza Mangungu.

Siku hiyo ambayo ligi ilimalizika na Simba kukabidhiwa kombe lao la ubingwa, miongoni mwa viongozi wa mabingwa hao ambao hawakupewa nafasi ya kuitwa na kuvalishwa medali ni Mangungu huku ikiibua maswali mengi.

Kwa upande wake Mangungu pamoja na kulalamika lakini alidai kuwa ufafanuzi zaidi wanao viongozi wa Bodi la Ligi (TPLB) kuwa kwanini hakupewa nafasi hiyo kama kiongozi wa klabu na kama ilivyo kwa viongozi wenzake.

Katika sherehe hizo, mtangazaji aliwaita viongozi wa Simba ambao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Dewji na Makamu wake Salim Abdalah 'Try Again' kuwa ndio wanaotakiwa kushuka kwenda kutoa zawadi kwa wachezaji wao.

Jambo hilo lilimfanya Mangungu akose kuvaa medali licha ya kuwepo uwanjani na jukwaa la watu maalum waliokuwa wanafuatilia mchezo wao ambao walishinda bao 4-0 dhidi ya Namungo.

Suala hilo limefafanuliwa na viongozi wa TPLB kupitia Afisa Habari wao, Karim Boimanda ambaye amesema jina la Mangungu lilikuwepo kwenye orodha ya watu waliotakiwa kuvalishwa medali hizo lakini huenda kuna jambo ambalo lilifanyika kimakosa na kutoitwa jina lake.

"Nadhani ni pande zote mbili zilifanya makosa ambayo ni ya kibinadamu tu, bodi huenda kosa letu ni kuzidisha medali za timu maana kawaida inatakiwa kutengeneza medali kwa ajili ya wachezaji na benchi la ufundi tu na si kwa kiongozi yeyote. "Hivyo tulizidisha medali ambapo Simba walitupa majina ya watu wanaopaswa kupewa hizo medali likiwepo jina la Mangungu, katika uvalishaji wa medali bodi haihusiki wanaohusika ni upande wa timu, hivyo huenda wao ndiyo walipitiwa na kutomwita Mangungu kwa ajili ya hilo.

"Lakini tunajifunza kutokana na makosa, kwani wakati mwingine medali zitakazandaliwa zitakuwa ni kwa wachezaji na benchi la ufundi pekee, watu wengine walikuwa wanapewa kama mazoea tu ila sio utaratibu na si kanuni," amesema Boimanda