Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 26Article 553897

Michezo Mingine of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Bodi ya Michezo ya Kubashiri yateketeza mashine 73 Mwanza

Tinga tinga likiharibu Mashine za Michezo ya kubashiri Tinga tinga likiharibu Mashine za Michezo ya kubashiri

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini, imeziharibu kwa kuzivunja vunja mashine 73 za michezo hiyo ambazo zilikuwa zikitumika bila kusajiliwa na bodi hiyo, huku nyingine zikikutwa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kisheria wakati wa msako maalumu uliofanyika mkoani mwanza.

Kwa hatua hiyo, wamekua wakiikosesha serikali mapato kwa kiasi kikubwa na wale wanaoendeleza michezo hiyo hatua kali zinakuja.

Bodi hiyo imesema huo ni mwanzo na wataendeleza msako kwa wote wanaoendesha shughuli hizo kinyume na taratibu za Serikali.