Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 05Article 541168

xxxxxxxxxxx of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Breaking: Kahata Aaga Rasmi Simba, Kusepa Sudan

KIUNGO wa kimataifa wa Kenya na klabu ya Simba, Francis Nyambula Kahata amewaaga rasmi mashabiki, uongozi, Benchi la ufundi na wachezaji wa timu hiyo huku akisema muda umefika wa kutafta changamoto mpya huku akiwashukuru kwa sapoti yao.

Taarifa zinadai kuwa, baada ya mkataba wake na Simba kumalizika, ameanza mazungumzo na Klabu ya El Merreikh ya Sudan, na hakuna taarifa yoyote ile ya Kusajiliwa na Klabu kutoka hapa Tanzania.Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kahata amesema; “Ninaondoka nikiwa kifua mbele huku najivunia mafanikio ndani ya klabu. Umefika wakati wa kusema kwaheri kwenu nyote. Natakiwa kutafuta changamoto mpya na nafasi sehemu nyingine” Francis Kahata, akiwaaga na kuwashukuru viongozi, wachezaji pamoja na mashabiki wa Simba.

It’s been a journey that is sweet, memorable and bitter since I first landed to this great country Tanzania. I received immense support and love from the executive team led by Mo Dewji,technical staff, playing unit and Wanasimba fans.

My gratitude goes to the head coach Didier Gomes for the opportunity to represent the Red color, my team mates for the impressive support and everyone who rode with me along the way. I leave with my head held up and proud of my achievements at the club.

It has reached a time to say good bye and bid farewell to all of you. A man has to seek newer challenges and greater opportunities elsewhere. I will forever be grateful to the team for everything and wish everyone all the best in the coming games and seasons. The 2 years were worth the ride.

Asanteni sana wanaSimba na kila la kheri hadi siku ingine palipo Majaliwa.

Kahata 25. ADIOS!Join our Newsletter