Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 29Article 560278

Soccer News of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Breaking: Mo Dewji ang'atuka Simba SC

Mohammed Dewji, ajiuzulu wadhifa wake ndani ya Simba Mohammed Dewji, ajiuzulu wadhifa wake ndani ya Simba

Mdhamini na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Simba Sports Club, Mohammed Dewji "Mo" amejiuzulu nafasi hiyo baada ya kikao na bodi ya wakurugenzi kukubaliana iwe hivyo.

Kikao hicho ambacho kimefanyika Septemba 21, mwaka huu kilikubaliana kuwa Mo aachie wadhifa huo.

Akizungumza "Mo" amesema;

"Sababu kubwa za kuachia nafasi hii ni kwa vile mimi ratiba zangu ni nyingi,na ninasafiri mara kwa mara hivyo nimeona ni busara niachie majukumu haya kwa watu wengine"

Mo ameongoza Bodi ya Wakurugenzi wa Simba kwa miaka minne na amewashukuru wanachama,wapenzi,viongozi na mashabiki.

Mo atabaki kuwa mdhamini na amewataka wanasimba wasiwe na hofu kwani ataendelea kushirikiana naSimba wakati wowote watakapohitaji msaada wake na atabaki kuwa mpenzi wa Simba mpaka siku ya mwisho.

Nafasi ya "Mo" kwa sasa itachukuliwa na aliekuwa mshauri wake, Salim Abdallah maarufu kama "Try again".