Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 25Article 544147

Habari za michezo of Friday, 25 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Breaking News: Adhabu Ya Mwakalebela Yatenguliwa na TFF

Mwakalebela Mwakalebela

Breaking News: Adhabu Ya Mwakalebela Yatenguliwa na TFF June 24, 2021 by Global PublishersMAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Fedrick Mwakalebela leo Juni 24, 2021 ameshinda kesi ya maombi ya marejeo mbele ya kamati ya maadili ya TFF  dhidi ya hukumu ya kufungiwa miaka mitano kujishughulisha na mpira wa miguu ndani na nje.

Kamati hiyo iliyoketi  Juni 23, imeridhia kumuondolea adhabu ya kifungo cha miaka mitano Pamoja na faini ya jumla ya sh. milioni saba.

Mwakalebela katika katika maombi yake amesema  anajutia kosa  hivyo anaomba aondolewe adhabu hiyo amabyo ameitii kwa kipindi chote, aliomba apewe fursa nyingine ya kutumikia  mpira wa miguu.