Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585709

African Cup of Nations of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Burjina Faso wapata ushindi wa Kwanza dhidi ya Cape Verde

Wachezaji wa Burkina Faso wakipongezana Wachezaji wa Burkina Faso wakipongezana

Burkina Faso imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa pili hatua ya makundi Kundi A uliopigwa dimba la Yaounde Cameroon.

Kwa ushindi huo Burkina Faso waafikisha alama tatu sawa na Cape Verde ingawa wanashika nafasi ya pili kutokana na goli za kufunga na kufungwa.

Goli lililoamua mchezo huo limefungwa na Boureima Bande kunako dakika ya 39 ya mchezo akimalizia mpira wa Issa Kabore.

Ukiwa ni mchezo mwingine tena kwenye AFCON 2021 ambao umeamuliwa na goli moja, Burkina Faso wanaweza kuwa na njia rahisi kiasi kutinga 16 bora kulinganisha na Cape Verde ambao mchezo wa mwisho watakutana na mwenyeji Cameroon wakipoteza watakuwa wanaaga rasmi mashindano hayo kwenye mechi za Jumatatu.