Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 13Article 585649

African Cup of Nations of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Cameroon sio wa kawaida AFCON, Waichapa Ethiopia 4

Cameroon wana uhakika wa kusonga hatua inayofuata Cameroon wana uhakika wa kusonga hatua inayofuata

Wenyeji wa michuano ya AFCON, Timu ya Cameroon wamekuwa timu ya kwanza kuingia hatua ya mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Ethiopia katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Paul Biya Jijini Yaoundé.

Mabao ya Cameroon yamefungwa na Karl Toko Ekambi mawili dakika ya nane na 67 na Vincent Aboubakar mawili pia dakika ya 53 na 55, baada ya Wahabeshi kutangulia kwa bao la Dawa Hottesa dakika ya nne.

Kwa matokeo hayo, Simba Wasiofungika wanafikisha pointi sita baada ya mechi ya mbili na kuendelea kuongoza Kundi A huku pia wakifuzu Hatua ya mtoano.