Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 09Article 584500

African Cup of Nations of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Cameroon waanza AFCON na ushindi dhidi ya Burkina Faso

Cameroon yaibuka na ushindi wa goli 2-1 Cameroon yaibuka na ushindi wa goli 2-1

Cameroon imepata ushindi wa kwanza wa goli 2-1 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2022 mbele ya mashabiki wa nyumbani ambao walijitoleza kwa wingi.

Burkina Faso walianza vyema baada ya kutangulia kupata bao bora na bao la kwanza kwenye mashindano ya mwaka huu kupitia kwa Gustavo Sangare lakini Cameroon walirudi vyema na kupata goli mbili moja ikiwa ni penati.

Nahodha wa wenyeji wa michuano Vincent Aboubakar alirudisha shangwe kwa mashabiki katika eneo maarufu la Yaounde kufuatia goli mbili kwa njia ya matuta.

Hata hivyo, Burkina Faso wameonyesha kandanda safi wakimlazimisha kipa wa Ajax Andre Onana kufanya kazi ya ziada kuokoa michomo langoni mwake.

Ushindi huo unaifanya Cameroon kuongoza kundi A kwa tofauti ya alama tatu na timu nyingine ambapo mechi ya baadaye Cape Verde wanacheza na Ethiopia.