Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 24Article 559447

Soccer News of Friday, 24 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Cedric Kaze, aliondoka kama dereva amerudi kama Kondakta

Kocha Cedrick Kaze Kocha Cedrick Kaze

Yanga inahusishwa kumrudisha aliewahi kuwa kocha wake mwanzoni mwa msimu uliopita 2020/2021 Mrundi Cedric Kaze.

Kaze alihudumu Yanga kwa kipindi kifupi Kabla ya kusitishiwa Mkataba wake yeye na benchi lake lote la Ufundi Machi 7 mwaka huu.

Kaze ni kocha mwenye wasifu mkubwa, ana Leseni Daraja A ya CAF, na anamiliki Leseni ya Chama Cha Soka Ujerumani, Deustcher Fussball Band (DFB), Kabla ya kutimuliwa Jangwani Kaze alihusika katika mechi 18 za Yanga msimu uliopita, alishinda mechi 10, kasuluhu mechi 7 na kupoteza mechi 1.

Kaze ameshawahi kubeba ubingwa wa Ligi kuu ya Burudi mwaka 2011, sio mtu wa mchezo na jambo kubwa zaidi ameshafundisha mpaka timu za Taifa za Vijana za Burundi chini ya miaka 17. 20 na 23.

Amefanya kazi mpaka katika Akedemi ya timu ya Barcelona, na analijua vyema soka la Afrika.

Yanga wanatajwa kumrudisha ili aje awe kkocha msadizi wa klabu hiyo iliyo chini ya Nasreddine Nabi. Kaze alipita Yanga kabla ya Nabi na kuwa kocha Mkuu leo anarudi kuja kuwa Kocha msaidizi.

Yani wakati anaondoka Yanga Machi mwaka huu ndio alikua mtu anaefanya maamuzi katika kila jambo linalohusu kikosi leo anarudi akiwa kama msaidizi, nyuma ya mtu mwenye maamuzi ya mwisho juu ya Kikosi cha Yanga.