Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573148

Habari za michezo of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Chama asimamisha kwa muda mkutano wa Simba

Chama asimamisha kwa muda mkutano wa Simba Chama asimamisha kwa muda mkutano wa Simba

Kiungo wa Berkane ya Morocco, Cletous Chama amesimamisha kwa muda hotuba ya Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo.

Wanachama walilipuka kwa furaha wakati Try Again alipowaeleza kumsajili mchezaji yoyote wanayemtaka baada ya mwekezaji wa klabu hiyo, Mo Dewji kumhakikishia mzigo upo.

Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' alipokuwa akizungumza na wanachama wa klabu hiyo leo katika mkutano mkuu wa Simba.

"Tutamleta yeyote, sijui awe Chama au nani, amesema Try Again na kushangiliwa kwa nguvu na wanachama wengine wakisimama na kutoa maneno ya kujisifu, hali iliyosababisha Try Again kusimama kwa sekunde kadhaa kusubiri wanachama wanalize kushangilia.

Kabla ya kumtaja Chama aliyeuzwa na klabu hiyo, Try Again alisema bodi ya Wakurugenzi imempa urais wa heshima Mo Dewji kwenye klabu hiyo kutokana na namna aluvyojitoa ndani ya klabu.

"Amenihakikishia pesa ipo, tutasajili yeyote tunayemtaka," amesisitiza Try Again kwenye mkutano huo unaoendelea jijini Da es Salaam.