Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 30Article 554269

Soccer News of Monday, 30 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Chama la Mexime laichapa Yanga

Mchezaji wa Cambiasso Sports Academy akijiandaa kuondosha mpira mbele ya Mchezaji wa Yanga Mchezaji wa Cambiasso Sports Academy akijiandaa kuondosha mpira mbele ya Mchezaji wa Yanga

Timu ya Vijana ya Yanga (U-20), imeshindwa kuonesha makali yake kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kuchapwa mabao 3-1, kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Cambiasso Sports Academy inayonolewa na kocha Mecky Mexime.

Katika mchezo huo ambao ni wa utangulizi wa tamasha la Yanga ‘Wiki ya Wananchi’ dakika 30 za kwanza zilimalizika kwa Cambiasso kuongoza kwa bao 2-0.

Kipindi cha pili kilirejea kwa Yanga kutafuta mabao ya kusawazisha huku Cambiasso wakiendelea walipoishia na dakika kama ya 60 hivi, waliongeza bao la tatu.

Dakika  ya 87, Yanga ilipata bao la kufutia machozi na kufanya mechi imalizike kwa 3-1.

Pamoja na kupoteza mchezo huo mashabiki wa Yanga waliopo uwanjani hapa hawapoi kwani walionekana kuishangilia timu yao kwa muda wote waliokuwa wakicheza.

Shamra shamra zinaendelea ndani ya Uwanja wa Mkapa ambapo leo ndio kilele cha tamasha la Yanga ‘Wiki ya Mwananchi’.