Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572608

Boxing News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Cheka, Alkasasu uso kwa uso ulingoni

Bondia Cosmas Cheka akimtambia mpinzani wake mbele ya waandishi wa habari Bondia Cosmas Cheka akimtambia mpinzani wake mbele ya waandishi wa habari

Wanamasumbwi wa ngumi za kulipwa nchini, Muksini Swalehe ‘Alkasusu’ na Cosmas Cheka wanatarajia kupanda ulingoni Desemba 3, mwaka huu katika pambano la usiku wa mishindo ambalo limepangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar.

Pambano hilo limetambulishwa leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika kwenye Hoteli ya Atriums ambalo litashirikisha mabondia wengi, limeandaliwa na Kampuni ya Grobox Sports Promotion nchini ya Siaha Mosha.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Promota wa pambano hilo, Siaha Mosha alisema kuwa wamezindua kampuni yao ambayo itakuwa inajihusisha na mambo ya burudani lakini kwa sasa wameanza na mchezo wa ngumi za kulipwa kwa kuwapiganisha Alkasusu na Cheka katika pambano la Desemba 3, mwaka huu.

“Kitu cha kwanza ni kwamba tumezindua na kuitangaza kampuni yetu ya Grobox Sports Promotion ambayo itakuwa ikihusisha na masuala ya burudani lakini kwa sasa tumeanza na mchezo wa ngumi ambao umekuwa mkubwa, tumeandaa pambano ambalo litawakutanisha Alkasusu na Cosmas Cheka kama pambano kuu.

“Pambano linatarajia kufanyika Desemba 3, mwaka huu na litajulikana kama usiku wa mishindo kwa sababu kila bondia anakishondo chake na kila mtu anataka kuacha historia, litakuwa ni pambano zuri na kubwa na litafanyika kwenye Uwanja Kinesi, Dar,” alisema Mosha.