Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 08Article 584335

Soccer News of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Chelsea yaichapa 5-1 Chesterfield Kombe la FA

Chelsea yashinda 5-1 Chelsea yashinda 5-1

Timu ya Chelsea imeibuka kidedea kwa ushindi wa bao 5-1 dhidi ya klabu ya Chesterfield katika mchezo wa Kombe la FA hatua ya tatu ambapo ushindi huo unaipeleka hatua ya nne.

Mchezo ukichezwa dimba la Stamford Bridge, The Blues walikuwa kwenye ubora mkubwa wakitawala mchezo vyema na kushuhudia mabao ya Timo Werner, Callum Hudson-Odoi, Romelu Lukaku, Andreas Christensen na Hakim Ziyech wakati lile la kufutia machozi likifungwa na Akwasi Asante.

Ndiyo wamepoteza, lakini inaweza kuwa furaha kwa wachezaji na mashabiki kwa kuwa karibu na wachezaji wakubwa mithili ya klabu ya Chelsea.