Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 25Article 559699

Soccer News of Saturday, 25 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Chelsea yapunguzwa kasi, yachapwa 1 na City

Mshambuliaji wa Man City akishangilia goli dhidi ya Chelsea Mshambuliaji wa Man City akishangilia goli dhidi ya Chelsea

Ngoma ikivuma sana hatimae hupasuka, ndivyo ilivyotokea kwa watoto wa London, Chelsea baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Manchester City katika uwanja wao wa nyumbani Stamford bridge katika muendelezo wa EPL.

Chelsea walianza msimu huu kwa ushindi wa Kombe la Super Cup, kisha wakacheza mechi 5 za ligi pasipo kupoteza, bila kusahau ushindi wao katika michuano ya Ulaya na Kombe la Carabao.

Kabla ya mchezo wake na Man City, rekodi zilikua zikimpendelea Chelsea kwani alicheza michezo mitatu mfululizo na Man city ikiwemo mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na katika mechi zote tatu aliibuka na ushindi.

Manchester City walikua katika kiwango bora kabisa huku wakitengeneza nafasi nyingi ambazo walishindwa kuweka mpira wavuni .

Goli pekee la Man City limefungwa na Nyota wa KIbrazil Gabriel Jesus 53' na kuwahakikishia City kuondoka na pointi tatu.