Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 07Article 541402

xxxxxxxxxxx of Monday, 7 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Chirwa anogewa Ligi Ligi Kuu Bara

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Chirwa mchezaji wa zamani wa Yanga, alisema yeye anajua kuwa mkataba wake unamalizika, lakini bado anaipa nafasi timu yake hiyo kwa ajili ya mkataba mpya, ila kama ikishindikana timu zipo nyingine nchini Tanzania.

"Suala la mkataba nawaachia viongozi. Mimi mwenyewe najua kuwa unakwisha, lakini naona bado nina nafasi kwa sababu mimi ni mzoefu sana na soka la Tanzania, nimecheza misimu mingi na nalifahamu, hivyo naamini Mungu akijaalia nitabaki Azam, lakini kama hakupenda basi timu hapa nchini zipo nyingi, nitaenda timu nyingine. Lakini kwanza kabisa naipa kipaumbele timu yangu ya Azam," alisema Chirwa.

Kwa maelezo haya ni kwamba Chirwa ana asilimia kubwa ya kubaki kucheza soka nchini Tanzania, ama kwa kuongezewa mkataba na klabu yake na kama sivyo basi ni wazi kuna timu za hapa hapa ambazo zinaonekana kumhitaji na yeye pia akitamani kuendelea kucheza soka Bongo.

Raia huyo wa Zambia alijiunga na Azam mwaka 2018 akitokea Nogoom FC ya Misri ambako aliyojiunga nayo muda mfupi tu baada ya kuondoka Klabu ya Yanga.

Chirwa alijiunga na Yanga mwaka 2016 akitokea Klabu ya FC Patinum ya Zimbabwe na kuichezea kwa misimu miwili kabla ya kutimkia Misri, baadaye kuibukia Azam FC, ingawa kwa sasa amekuwa hapati sana nafasi ya kucheza chini ya Kocha Mkuu Mzambia mwenzake, George Lwandamina.

Join our Newsletter