Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 31Article 554641

Soccer News of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Coastal Union yaja na Mkakati wa Kufanya vyema Ligi kuu

Melis Medo, Kocha mpya wa Coastal Union Melis Medo, Kocha mpya wa Coastal Union

Katika mkakati wa kuhakikisha wanafanya vyema kwa msimu ujao, Klabu ya Coastal Union ya Tanga imeingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Mmarekani, Melis Medo kuinoa timu hiyo.

Medo anachukua nafasi ya Juma Mgunda ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 1988.

Taarifa ya Coastal Union imesema kwamba aliyekuwa msaidizi wa Mgunda, Joseph Lazaro ataendelea kuwa Kocha Msaidizi wa Medo.

Medo alikuwa Kocha wa Gwambina kuanzia Mei mwaka huu baada ya kufundisha klabu kadhaa nchini Kenya ikiwemo Wazito na Sofapaka.

Kwa misimu takribani miwili Klabu ya Coastal Union imekua dhofu lihali kwa namna inavyomaliza ligi kuu na ikumbukwe msimu uliopita walicheza michezo ya mtoano kuhakikisha wanabaki Ligi Kuu.

Hivyo katika kuliona hilo wameamua kuhakikisha wanaongeza nguvu na kufanya vyema msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara.