Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584962

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Conte aiota Fainali ya Carabao Cup

Kocha wa Spurs, Antonio Conte Kocha wa Spurs, Antonio Conte

Kocha wa Tottenham Antonio Conte ana kazi kubwa ya kuweza kupindua matokeo ya 2-0 baada ya kupoteza dhidi ya timu yake ya zamani Chelsea kwenye mchezo wa nusu Fainali ya Carabao Cup.

Chelsea tayari wamepiga hatua moja mbele kwenye hatua ya fainali kufuatia ushindi walioupata kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Carabao Cup, kufutuatia kuibuka na ushindi kwenye dimba la nyumbani Stamford Bridge wiki iliyopita huku timu zote zikiwa na idadi ya wachezaji kladhaa ikiwakosa.

Conte tayari alishathibitisha kuwa mshambuliaji wake hatari msimu huu Heung-min Son, hatakuwepo kwa wiki nne kutokana na majeruhi, hivyo hana budi kuwatumia Harry Kane na Lucas Moura kwenye safu ya ushambuliaji huku katikati akiwajumuisha Pierre-Emile, Hojbjerg na Oliver Skipp pia anatarajia beki wake Eric Dier kurudi baada ya kupona jeraha.

Huku klabu ya Chelsea ikionekana dhahiri kuwa itacheza kwa kujiamini zaidi japo haitakuwa na kipa wake Mendy ambaye yuko AFCON, pia kuna wasiwasi kama N’Golo Kante na Thiago Silva watacheza baada ya kukutwa na maambukizi ya Uviko-19 kwenye mchezo wa kwanza.