Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 14Article 563152

Soccer News of Thursday, 14 October 2021

Chanzo: ippmedia.com

Courtois aishutumu FIFA, UEFA

Golikipa wa Ubelgiji na Real Madrid Golikipa wa Ubelgiji na Real Madrid

Ubelgiji ilicheza na Italia katika kutafuta mshindi wa tatu kwenye michuano ya Ligi ya Mataifa ya Uefa, ambapo ilifungwa, kabla ya mchezo wa fainali ambao ulizikutanisha Ufaransa na Hispania.

Na sasa Thibaut Courtois ameishutumu FIFA na UEFA kwa kujali fedha pekee.

“Ni mchezo wa fedha tunapaswa tuwe wakweli kuhusu hili,” alisema Courtois akiwaambia waandishi wa habari.

“Tumecheza huu mchezo ni kwa sababu ya UEFA, fedha ya ziada na mchezo wa ziada kwenye TV.

“Tutapata majeraha, hakuna anayejali wachezaji, baada ya msimu mrefu unatakiwa tena kucheza Ligi ya Uefa na utakuwa na wiki mbili za mapumziko hiyo haitoshi kwa wachezaji.

“Wanaweza kuchukizwa na Super League, lakini hawajali kuhusu wachezaji wanajali mifuko yao tu. Sisi siyo maroboti.”