Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 30Article 554398

Habari za michezo of Monday, 30 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

DTB Wamepania Ligi Kuu, Tambwe Ndani

DTB Wamepania Ligi Kuu, Tambwe Ndani DTB Wamepania Ligi Kuu, Tambwe Ndani

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC na Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya DTB FC ambayo msimu ujao itacheza Championship.

Tambwe alitambulishwa hivi karibuni kuwa mchezaji wa DTB ambapo ataungana na mastaa wengine kama Juma Abdul, David Mwantika na Yannick Bazola ili kukiimarisha kikosi hicho kilichopania kucheza Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTB FC, Muhibu Kanu, alisema: “Maandalizi mpaka sasa yapo vizuri na tumemsajili Tambwe na nyota wengine, hadi sasa timu tayari ipo kambini ikiendelea na mazoezi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar, ambao pia tutautumia kama uwanja wetu wa nyumbani kwenye ligi.

“Tumekwisha maliza kusajili na mpaka sasa tuna wachezaji 26 ambao kati yao wachezaji sita ni wa kigeni, mpango wetu kwa sasa ni kuhakikisha tunafanikiwa kufika ligi kuu.”Imeandikwa na Onesmo Milanzi (SJMC), Jonas Makore na Richard Ngailla (Tudarco)

Share this:TweetWhatsApp Related