Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572554

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Dembele ni mchezaji wa kipekee sana – Dani Alves

Ousmane Dembele Ousmane Dembele

Meneja wa Barcelona Xavi Hernandez na mlinzi anayerejea, Dani Alves wanakubaliana na uhalisia kuwa Ousmane Dembele ni mchezaji muhimu na wa pekee Barcelona. Barcelona inaendelea na mazungumzo juu ya mkataba wa staa huyu.

Dembele amekuwa akikwama kwenye changamoto ya majeraha tangia alipowasili klabuni hapo kwa uhamisho wa zaidi ya €100m, akitokea Dortmund mwaka 2017.

Kutokana na changamoto ya majeraha staa huyu mwenye umri wa miaka 24 ameshindwa kufikia matarajio ya wengi klabuni hapo. Hata hivyo, Xavi anaamini nyota huyu ni sehemu muhimu ya mipango yake Barcelona.

Hata hivyo, Xavi na Alves wanakiri kuwa nyota huyu bado ana umuhimu mkubwa klabuni hapo, na anahitaji kupewa muda ili aweze kufanya vizuri zaidi.

“Dembele kwa nafasi yake anaweza kuwa mchezaji bora duniani. Anahitaji kuwa na viwango kama mchezaji wa kimataifa. Ni muhimu kuwa na mtazamo wa ushindi. Tunahitaji kumsaidia.” – Xavi

Dani Alves, akiwa anarejea klabuni hapo alizungumza na vyombo vya habari juu ya mtazamo wake juu ya Dembele.

“Dembele ni mchezaji wa kipekee sana. Anahitaji tu kutambua yeye ni mwana Barca, na kuamini kuwa yeye ni mchezaji mkubwa na anaweza kufanya mambo makubwa.” amesema Dani Alves