Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585193

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Denis Nkane Yamemkuta Yanga

Denis Nkane Yamemkuta Yanga Denis Nkane Yamemkuta Yanga

KIUNGO Mshambuliaji waYanga, Denis Nkane atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na Kinena.

Nkane alisajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili akitokea Biashara United, huku kwa sasa akiwa amecheza mechi mbili za michuano ya Mapinduzi.

Kiungo huyo aliumia kwenye mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya KMKM kwenye Kombe la Mapinduzi.

Daktari waYanga, Youssef Mohammed, alisema kuwa: “Kwa sasa kuna jumla ya wachezaji wanne ambao ni majeruhi kwenye kikosi.

“WapoYacouba Sogne, Kibwana Shomari,Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambao wanaenda Tunisia kwa ajili ya kupatiwa matibabu na Denis Nkane.

“Denis alipata majeraha kwenye mchezo wa mwisho wa makundi ambapo kwa sasa anasumbuliwa na Kinena, tatizo ambalo litamuweka nje kwa muda wa mwezi mmoja.”