Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572848

Boxing News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Dillian Whyte amtaka Tyson Fury ulingoni

Tyson Fury (kushoto) na Dillian Whyte Tyson Fury (kushoto) na Dillian Whyte

Mcheza masumbwi wa Muingereza, Dillian Whyte amesema bingwa wa IBF, WBO na WBC, Tyson Fury hana chaguo zaidi ya kukubali masharti ya WBC kupigana nae.

Tayari WBC wametoa taarifa mbele ya hadhara kwamba Fury apambane na Dallian Whyte ambaye ni bingwa wa muda wa WBC, endapo hataweza kukubali kupigana katika pambano la ubingwa wa dunia dhidi ya Oleksandr Usyk ndani ya siku 30.

Pamoja na muda wa mwisho kufika, WBC bado hawajatangaza pambano linalofwata la Fury katika mkutano wa mwaka, lakini Whyte ameweka wazi masharti yameshawekwa na uongozi wa serikali.

“Tayari imethibitishwa kwamba Tyson Fury lazima apigane na mimi kwanza,” Dillian Whyte

“Taarifa imetolewa katika wavuti yao kwamba mimi ndie changamoto yake mpya na mpiganaji wa pambano linalofwata la Tyson Fury.”

“Sielewi hizi changamoto zimetokea wapi. Yeye [Fury] anajaribu kutaka kupambana na Usyk, kwasababu Usky ni pambano rahisi zaidi kwake.

“Fury alichagua kupambana na mimi mara mbili. Aliomba WBC mkanda wa Diamond ili apigane na mimi, lakini alikimbia baada ya kukubaliana. Anazidi kutengeneza sababu.” aliongeza Dillian Whyte.