Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 09Article 584365

Tennis News of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Djokovic aliruhusiwa Kucheza Australian Open

Mcheza Tennis, Novac Djokovic Mcheza Tennis, Novac Djokovic

Nyota wa tenisi Novak Djokovic alikuwa na msamaha wa chanjo ya kuingia Australia baada ya kuambukizwa Covid mnamo 16 Desemba, mawakili wake walisema katika hati za mahakama.

Djokovic alinyimwa kuingia Australia baada ya kutua Melbourne wiki hii kucheza michuano ya wazi ya Australian Open.

Mchezaji tenisi huyo anayeshikilia namba moja duniani kwa sasa yuko katika kizuizi cha wahamiaji kabla ya kufunguliwa kesi mahakamani siku ya Jumatatu.

“Bw Djokovic alipokea barua, tarehe 30 Desemba 2021, kutoka kwa Afisa Mkuu wa Tiba wa Tennis Australia iliyorekodi kwamba alikuwa amepewa ‘msamaha wa kimatibabu kutoka kwa chanjo ya COVID’ kwasababu alikuwa amepona COVID hivi karibuni,” ilisomeka barua hiyo.

Kesi yake imezua kilio kikubwa nchini Australia na kushika vichwa vya habari duniani kote.

Wakati huo huo picha zimeibuka za Djokovic akionekana kuhudhuria hafla katika mji mkuu wa Serbia Belgrade wakati alipopimwa.

Mshindi wa pili wa michuano ya Australian Open, Renata Voracova kutoka Jamhuri ya Czech, sasa ameondoka nchini baada ya kufutwa kwa visa yake.