Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 28Article 560152

Soccer News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Dodoma Jiji yawapigisha kwata maafande wa Ruvu

Kipute cha Dodoma Jiji dhidi ya Ruvu Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Kipute cha Dodoma Jiji dhidi ya Ruvu Uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Timu ya Soka ya Dodoma Jiji imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri baada ya kuwakandamiza maafande wa Ruvu Shooting bao 1-0.

Katika mchezo huo uliopigwa majira ya mapema kabisa (saa 8:00 mchana) ulishuhudia Ruvu shooting wakiondoka mikono mitupu licha ya siku chache zilizopita, kupitia kwa Afisa Habari wake, Masau Bwire kujinasibu kuwa hakuna atakaepata pointi dhidi yao.

Goli la pekee katika mechi hiyo limewekwa wavuni na Cleophance Mkandala dakika ya 33 ya mchezo na kuwafanya Dodoma JIji kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele.

Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji inakwenda nafasi za juu wa msimamo wa Ligi kuungana na Mbeya Kwanza na Namungo FC ambazo nazo pia zilishinda michezo yake siku ya Jana.