Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585340

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Du! kumbe Simba ilifanya umafia kwa Sakho

Pape Ousmane Sakho Pape Ousmane Sakho

Mjumbe Kamati ya Usajili na Mshauri wa Aliyekuwa M/Kiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Crescentus Magori ameeleza namna walivyomnasa Pape Ousmane Sakho.

“Niliwaambia watu kuwa Sakho alikuwa anaenda kwenye majaribio timu moja ya Uturuki ya Premier tukaingilia kati kumnunua akiwa na tiketi mkononi watu walijua napiga hadithi tu!” alianza Magori.

“Huyu mchezaji asingeumizwa siku ile Dodoma, sasa hivi angekuwa wa moto zaidi ya sasa hivi.

“Ni uamuzi wake. Ilikuwa aende majaribio Transpoor ya Turkey, ambayo hayana uhakika, au aje Simba ambapo ilikuwa na uhakika wa usajili! Akaamua kuacha trial akaja kusajiliwa Simba.

“Na Rais wa Klabu yake aliweka kipengele cha onward sale percent iwapo mchezaji atauzwa!!” aliongeza Magori.

Sakho ataiongoza Simba SC katika fainali ya kombe la Mapinduzi Zanzibar hapo kesho watakapo vaana na Azam FC katika uwanja wa Karume majira ya saa mbili na robo usiku.