Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558355

Soccer News of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Emmanuel Okwi ndani ya Simba Day, asema chochote kinaweza tokea

Mchezaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi (mwenye jezi nyeupe) Mchezaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi (mwenye jezi nyeupe)

Mchezaji wa zamani wa Simba SC, Emmanuel Okwi ameamsha shangwe kwa Mashabiki wa Simba waliofurika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia kilele cha Tamasha la Simba Day.

Okwi ambae ni kipenzi cha Mashabiki wa Simba Sports Club amesema amekuja kama shabiki wa Simba na amekuja kupongeza kitu kikubwa ambacho kinafanywa na klabu hiyo.

Alipoulizwa kuhusiana na tetesi za yeye kurejea Simba amesema yeye ni mchezaji kwa sasa ambae yupo huru (hana mkataba na klabu yoyote) na soka ndio kazi yake hivyo chochote kinaweza kutokea.

Kuna uvumi ama tetesi zinazungumzwa kuwa Okwi atarejea msimbazi pindi dirisha dogo , Januari litakapofunguliwa.

Okwi amezunguka uwanja mzima akiwasalimia mashabiki na wanachama wa Simba walifurika Uwanja wa Mkapa kushuhudia timu yao ikicheza na TP Mazembe.