Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 22Article 573496

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Evra atoa maneno ya faraja kwa Ole Gunnar Solskjaer

Patrick Evra Patrick Evra

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Patrice Evra ambae pia ni mchezaji mwandamizi wa Klabu hiyo aliyewahi kucheza pamoja na Christiano Ronaldo pamoja na Ole amemshukuru Ole Gunnar Solskjaer kwa kazi yake na amewapa kitisho wachezaji wa Manchester United akisema “ninakuja nyuma yenu”

Evra ameandika katika mtandao wa instagram

”Asante rafiki yangu kwa kutufanya tuiamini tena Manchester United. Kwa bahati mbaya usipopata matokeo watu husahau mazuri uliyoyafanya. Kwa wachezaji wote wa Manchester United ninakuja, tuonane katika mechi na Arsenal “.

Evra alikuwa mchezaji mwenzake na Solskjaer wakati wa msimu wa mwisho wa Ole akichezea Manchester United. Wote kwa pamoja walikuwa chini ya Sir Alex Ferguson.