Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 22Article 573451

Michezo Mingine of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

F1: Lewis Hamilton aendeleza alipoishia Sao Paulo

Lewis Hamilton Lewis Hamilton

Nyota wa mbio za magari Lewis Hamilton alishinda Qatar Grand Prix huko Losail International Circuit siku ya Jumapili akimshinda mpinzani wake wa Red Bull Max Verstappen.

Hamilton aliongoza kutoka kuanza mpaka kumaliza wakati Verstappen alipata penati ya 5-place baada ya kukiuka sheria ya bendera ya njano katika kufuzu, na aliweza kupanda hadi nafasi ya pili baada ya kuanza mbio tena katika nafasi ya saba.

Dereva aliyevutia zaidi alikuwa Fernando Alonso wa Alpine, ambaye alifanikiwa kumaliza mbio hizo katika nafasi ya tatu. Ilikuwa siku nzuri kwa timu ya Ufaransa, kwani Esteban Ocon pia alifanikiwa kumaliza katika nafasi ya tano.

Mtu ambaye alingeweza kuleta mjadala kuwa Driver of the Day, tuzo ambayo Alonso alishinda, ni Sergio Perez wa Red Bull, kwani alianza katika nafasi ya 11 na kumaliza katika nafasi ya nne.

Matokeo hayo ya Qatar Grind Prix yanamaanisha kuwa Verstappen bado ndiye kinara katika mbio za ubingwa baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 351.5, lakini Hamilton hayuko nyuma sana kwa pointi 343.5. Kuna mbio mbili tu zilizo salia, kwa hivyo shinikizo ni kubwa.

MSIMAMO WA 5 BORA ZA MADEREVA

1. Max Verstappen (Red Bull) 351.5

2. Lewis Hamilton (Mercedes) 343.5

3. Valtteri Bottas (Mercedes) 203

4. Sergio Perez (Red Bull) 190

5. Lando Norris (McLaren) 153