Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 12Article 551140

Soccer News of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Fainali Kagame ni vita ya Uganda, Malawi

Wanafainali wa Kagame Cup, Express FC Wanafainali wa Kagame Cup, Express FC

Mashindano ya Vilabu Afrika Mashariki na kati,Cecafa Kagame Cup kwa msimu huu yatafika tamati kesho kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya mchezo wa fainali kumalizika utakaozikutanisha timu za Express ya Uganda na Nyasa Big Bullets ya Malawi.

Timu hizo mbili zilizotinga fainali, zilifuzu kucheza nusu fainali kutokea kundi A, lililokuwa na timu nyingine za Yanga (Tanzania) na Atlabara ya Sudan kusini.

Katika mechi za nusu fainali, Express ilikutana na KMKM ya Zanzibar na kushinda kwa mabao 2-0 kisha kutinga fainali huku Nyasa Big Bullets wakiiondosha Azam kwa mikwaju ya penalti 4-2, baada ya dakika 120 za nusu fainali kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Hii itakua fainali ya tatu kwa Express ya Uganda baada ya kufanya hivyo mara mbili mfululizo mwaka 1994 na 1995, ambapo mara zote ililikosa kombe hilo hivyo itakuwa na uchu wa kulibeba kwa mara ya kwanza.

Kwa upande wa Nyasa ni mara ya kwanza kufika fainali, pia ni mara ya pili kwa timu kutoka Malawi kufika fainali ya mashindano hayo baada ya ADMARC Tigers kufika fainali mwaka 1983.

Kwa maana hiyo ushindani katika mchezo huo utakuwa mkubwa kulingana na timu zote mbili kutaka kubeba kombe hilo kwa mara ya kwanza.